Skip to content

SIG-III

The Special Interest Group for International Information Issues (SIG/III) is an interest group focusing on international information issues.

See this page in your own language: العربية (Arabic)中文(Chinese) | English | Italiano (Italian) فارسی (Persian) | Kiswahili (Swahili)

Kuhusu SIG-III

SIG-III ni Kikundi Maalum cha wapenda habari tofauti tofauti za Kimataifa. Kikundi hiki kilianzishwa mwaka wa 1982. Lengo kuu la kikundi hiki (SIG-III) ni kutumia Dhamira, Dira na Maadili ya Chama cha Sayansi na Teknolojia (ASIS&T) kwa muktadha wa kimataifa. SIG-III inalenga kufikia malengo yafuatayo: a) Kuongeza uelewa miongoni mwa wanachama wa ASIS&T na wataalamu wa habari juu ya umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa. b) Kurahisisha na kuboresha mawasiliano na uhusiano miongoni mwa wanachama wa ASIS&T ulimwenguni kote katika masuala mbalimbali ya habari. c) Kuanzisha jukwaa la kuchunguza, kujadili na kuchambua kwa kina changamoto na maswala yote ya habari za kimataifa. Katika kutekeleza malengo haya, SIG imekusanya makundi tofauti tofauti ya  watafiti na watendaji kutoka sehemu mbalimbali duniani ili kuchunguza nyanja tofautitofauti za masuala ya habari za kimataifa.

 

Dira

Kuunda jumuia yenye nguvu na misingi imara katika kutoa huduma za kitaalamu juu ya taarifa  mbalimbali za kimataifa kwa kuboresha ushirikiano, mawasiliano na heshima miongoni mwa SIG-III.

Dhima

Kuwakilisha na kuwahudumia wanajumuia kwa kuwajengea uwezo wa kitaaluma na maarifa. 

Maadili

  • Tunazingatia usawa, haki, ushirikishwaji, na upekee katika mipango na shughuli zetu zote.
  • Tunaheshimiana na kujaliana sisi kwa sisi na jamii nzima.
  • Tunahimiza uwazi, udadisi,ubunifu na uvumbuzi. 
  • Tunahakikisha kuwa msingi wa mipango na shughuli zetu kuwa imara na endelevu.

Learn More

people

How to Join

To be a member, one first needs to be a member of the Association for Information Science & Technology (ASIS&T). When completing the Membership Application Form, select the special interest group (SIG) of your choice.

Apply Today